Fahamu

Teksi zageuka shamba la mboga za majani baada ya madereva kukosa kazi kisa Corona

Katika maegesho ya gari nchini Thailand katika mji mkuu wa Bangkok, utaona mbogamboga zikiwa zimeota katika paa ya magari ya kukodi ambayo yana rangi mbalimbali za kung’aa.

Vizuizi vikali vilivyowekwa nchini Thailand dhidi ya Covid-19 vimesababisha mji huo ambao ulikuwa na hekaheka nyingi kuwa na utulivu, na kufanya madereva wa teksi kukosa kazi.

Baada ya kukosa wateja, madereva wengi waliondoka mjini na kwenda nyumbani kwao vijijini, na kuacha kile kilichoitwa makaburi ya taksi.

Na sasa kampuni moja imeamua kutumia paa za magari hayo ambayo hayafanyi kazi kama shamba la kulimia mbogamboga, ambapo wanatarajia wanaweza kusaidia kuwalisha madereva na wafanyakazi wengine.

Thai staff members of the Ratchaphruek Taxi Cooperative water their community vegetable garden that was built on top of out of use Thai taxis on September 13, 2021 in Bangkok, Thailand.

A staff member water vegetables on the roof of a car.

Wafanyakazi wa taksi za ushirika wa Ratchaphruek wametengeneza bustani ya mbogamboga kwa kuweka udongo juu ya karatasi nyeusi za plastiki.

Wamepanda mbegu mbalimbali za mboga kama pilipili , matango na zukini.

Wana matumaini kuwa baada ya kuwasaidia madereva, chakula chochote kitakachosalia kitauzwa sokoni.

The son of a Thai staff members of the Ratchaphruek Taxi Cooperative waters their community vegetable garden that was built on top of out of use Thai taxis on September 13, 2021 in Bangkok, Thailand.

A row of abandoned taxis in Bangkok,

Biashara ya taksi mjini Bangkok kwa kawaida inategemea utalii katika sehemu kubwa lakini marufuku yaliyowekwa ya kuzuia wageni kuingia nchini humo ina maana kuwa karibu kila kitu kimesimama.

“Hili ndilo chaguo letu la mwisho,” Thapakorn Assawalertkun, mmoja wa wamiliki wa kampuni aliwaambia wakala wa habari AFP, aliongeza kusema kuwa magari mengi yana mkopo mkubwa bado ambao hawajamaliza kulipa.

“Kuotesha mboga za majani katika paa la taksi hakutaharibu magari hayo kwa kuwa kuna mengine ambayo yameshahairibika na hayawezi kutengenezeka . Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika,”alisema.

A view of the parking lot turned community garden at the Ratchaphruek Taxi Cooperative, where they're using taxi roofs as vegetable planters on September 11, 2021 in Bangkok, Thailand.

A worker watering plants on the roof of an abandoned taxi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents