Habari

Tetemeko la ardhi laua 56 Indonesia

Watu 56 wamekufa na wengine 700 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi la 5.6 katika kipimo cha Richiter kulikumba eneo la karibu na mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Picha za televisheni zimeonyesha uharibifu mkubwa wa mji wa Cianjur, ikiwemo barabara na nyumba zilizoharibiwa vibaya.

Meya wa mji huo Herman Suherman amesema kuna uwezekano idadi ya waliofariki ikaongezeka. Suharyanto, mkuu wa wakala wa kitaifa wa kukabiliana na majanga, amesema wahanga wengi waliangukiwa na vifusi kutoka kwa nyumba zao zilizobomoka.

Related Articles

Back to top button