HabariMichezo

TETESI: Kocha Mkuu wa Simba SC ndiyo huyu

Mabingwa mara nne mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara na Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati Simba SC wamehusishwa na Kocha Josef Vukusic (57) raia wa Slovakia.

Tetesi zilizopo ni kuwa, Josef Vukusic mwenye UEFA PRO Licence ana nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Kocha Pablo Franco aliyemalizana na Simba SC wiki kadhaa zilizopita.

Kwa sasa Kocha Josef anakinoa kikosi cha klabu ya Kosice ya Slovakia, ambapo amekiongoza katika michezo 33 akishinda mechi 19 akipata Sare 5 akipoteza 9.

Mkali huyo ambaye ni Muumini wa mfumo wa kushambulia zaidi hasa akitumia 4-3-3 Barani Afrika amefundisha klabu 4 (Al ahly Benghazi, Cape Town City, Polokwane City F.C na Amazulu) huku akiwa na uzoefu na soka la Afrika.
Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button