Michezo

TETESI: Kocha Noureddine Al-Nabi atua Yanga

Mabingwa wa Kihistoria, Timu ya Wananchi, Vijana wa Jangwani na Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young African Sports Club wanadaiwa kumpa mikoba Kocha, Nasreddine Nabi iliyoachwa na mtangulizi wake Cedric Kaze.

Nasreddine Nabi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya El Merreikh atachukua nafasi hiyo ambayo kwa sasa inakaimiwa na Juma Mwambusi.

Kwa mujibu wa tetesi zilizopo ni kuwa Kocha huyo Mpya wa #yangasc anatarajiwa Kuwasili rasmi Nchini hapo kesho siku ya Jumanne akiwa na benchi lake la ufundi.

Kocha huyo raia wa Tunisia ni muumini wa mfumo wa 4-1-4-1 na anauzoefu na soka la Afrika.

IMEANDIKWA NA @fumo255 @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents