HabariMichezo

TETESI: Simba,Yanga zajitosa kuwania saini ya kinda hili

Wakati dirisha dogo la usajili likiwa linakaribia kumekuwa na tetesi za hapa na pale kwa baadhi ya wachezaji wakihusishwa na Timu kubwa za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwemo Simba na Yanga.

Jina ambalo limeibuka ghafla na kuhusishwa kuwaniwa na Miamba hii ya soka Afrika Mashariki na Kati ni kinda, Ladack Chasambi.

Kwa mujibu wa Ufm radio, CEO wa Mtibwa Sugar, Swabri amefunguka namna watani hawa wa jadi walivyogonga hodi kuinasa saini ya Chasambi.

“Simba na Yanga wote wamegonga hodi Mtibwa Sugar kutaka kumsajili Ladack Chasambi. Tumeshawatajia dau la mchezaji wetu mwenye mkataba, kwahiyo wajipange waje mezani tumalizane.” Ufm radio, CEO wa Mtibwa Sugar, Swabri

Ladack Chasambi amekuwa na umaarufu baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa vijana walio chini ya miaka 2o (U-20)  msimu wa mwaka 2021/22.

Kinda hili la Mtibwa Sugar ameichezea timu ya taifa ya Tanzania karibia ngazi zote, kwa maana ya U15,U17,U20,U23

Anaandika @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents