TETESI: Usajili Simba, Yanga, Azam na klabu nyingine Vpl 2021/22

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam Sports Federation Cup, Serengeti Lite Women Premier League na michuano mingine ikiwa imemalizika huku baadhi ya Makocha na Wachezaji wakiwa likizo, Viongozi wa klabu mbalimbali wana haha katika usajili ili kuhakikisha wanaboresha vikosi vyao pale palipokuwa na mapungufu ili kutimiza malengo waliyojiwekea kwenye michuano mbalimbali iwe ya kitaifa ama ya kimataifa.

Zifuatazo ni TETESI za Usajili kwa Klabu za hapa Nchini Tanzania.

Yanga: Mshambuliaji wa DR Congo, Fiston Mayela (27) amesajiliwa na Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kandarasi ya miaka miwili.

Yanga: Mchezaji wa Biashara United, Yusuph Athuman (21) anatarajiwa kutambulishwa katika klabu hiyo ya Wananchi muda wowote kuanzia sasa.

Simba: Winga kutoka Malawi kinda wa miaka 20, Peter Banda yupo Nchini kukamilisha dili la kujiunga na Mabingwa wa Nchi Wekundu wa Msimbazi.

Azam: Imemsajili mkataba wa miaka miwili Mshambuliaji wa DRC Congo, Idris Mbombo.

Mbombe (24) anakuja kuiongezea nguvu Azam FC baada ya kufanya makubwa katika klabu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors.

Yanga: Makambo ametua Nchini kukamilisha dili la usajili katika timu ya Wananchi Yanga SC, picha mbalimbali zimeenea katika mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa Dar.

Yanga: Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa UD Songo kutoka Msumbiji, Jimmy Julio Ukonde (24) ametua Nchini kukamilisha usajili Jangwani.

Yanga: Mchezaji Dickson Ambundo (25) wa Dodoma Jiji muda wowote kutangazwa kujiunga na Young Africans Sports Club

Tetesi za usajili vpl 2021/22 zimeandikwa na Hamza Fumo Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button