Tetesi za soka barani Ulaya, Mshambuliaji Liverpool atabiri Ole Gunnar Solskjaer kutomaliza msimu, Arsenal kung’oa kiungo wa Barce 

Arsenal inataka kumsaini winga wa Barcelona Malcom, 22, huku Everton ikiwa tayari imewasilisha ofa ya dau la £31.5m kumsaini raia huyo wa Brazil. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Dean Saunders anaamini kwamba Ole Gunnar Solskjaer hatomaliza msimu huu kama mkufunzi wa Manchester United . (talkSPORT)

Solskjaer ana matumaini atafanikiwa kumnunua beki wa leicester Harry Magwire mbele ya majirani za wao wakuu Manchester City. (Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uhispania Juan Mata, 31, amekataa mshahara wa £550,000 kwa wiki kutoka kwa klabu ya Shanghai SIPG na akaamua kuandikisha kandarasi mpya na klabu hiyo ya Old Trafford. (90Min)Juan Mata

Mata anasema kuwa alitia saini kadarasi mpya kwa kuwa klabu hiyo ni miongoni ma klabu kubwa nne duniani. (MUTV)

Ofa ya Everton ya dau la Yuro 30m limekataliwa na Juventus kumnunua mshambuliaji wa Itali Moise Kean. (Tuttosport, via Sport Witness)

Newcastle United ilimpatia mkufunzi Sam Allardyce ofa ya kurudi na kuifunza klabu hiyo wiki iliopita , lakini alikataa fursa hiyo.. (Mail)Moise Keane

Roma Ina hamu ya kumsajili beki wa Tottenham Toby Alderweireld na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ana kifungu cha kumuachilia chenye thamani ya £25m . (Sky Sports)

Everton imewasilisha ombi la kumsaini mshambuliaji wa Lille Nicolas Pepe. Mchezaji huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24 ataigharimu the tofees dau litakalovunja rekodi la £58.5m. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Southampton ,25 Mario Lemina, ambaye anatakiwa na Man United Arsenal na Leicester, amesema kuwa hataki kuichezea klabu hiyo msimu ujao.. (France Football, via Daily Echo)Dani Cebalos

Tottenham wanaimarisha ombi lao la kutaka kumsaini kiungo wakati wa Real Madrid Dani Ceballos, 22, kwa mkopo. (Mirror)

Arsenal inajiandaa kuongeza mabeki Calum Chambers, 24, Carl Jenkinson, 27, ama kiungo wa kati Mohamed Elneny, 26, katika makubaliano ya kumsaini winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha. Ombi la The Gunners la £40m kumnunua mchezaji huyo 26 limekataliwa . (Mirror)

Manchester City iko tayari kumzuia kiungo wa kati Fabian Delph msimu huu licha ya uvumi unaomuhusisha mchezaji huyo mwernye umri wa miaka 29 na uhamisho wa kuondoka Etihad. (Metro)

David Luiz anaamini kwamba kurudi kwa Frank Lampard katika klabu ya Chelsea utaifanya klabu hiyo kutambua umahiri wake.. (Standard)

Related Articles

Back to top button