Tetesi za Soka Tanzania

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikielekea ukingoni kumekuwa na tetesi mbalimbali zinazohusiana na mchezo pendwa wa soka nchini.

Inadaiwa Simba SC imekamilisha usajili wa beki wa kushoto kutoka katika klabu ya Ruvu Shooting, Edward Manya mwenye umri wa miaka 27, licha mabingwa hao wa Nchi kutotoa taarifa rasmi lakini tetesi zilizopo kwa sasa kila kitu kipo sawa.

Mtangazaji wa Efm na TVE Oscar Oscar amechukua fomu ya kuwania Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Oscar anatamani kurithi kiti cha Wallace Karia ambaye pia yupo katika kinyang’anyiro hicho.

Tetesi zilizopo ni kuwa moja ya klabu za Ligi Kuu ya Wanawake imemuwekea dau nono Kocha wa Yanga Princess, Edna Lema (Mourinho) ili kupata huduma ya dada huyo ambaye amekuwa na sifa kubwa katika uwezo wake wa kuwanoa wachezaji wa kike kwenye soka la Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia hapo jana alichukua fomu ya kutetea kiti chake cha urais ndani ya TFF baada ya uongozi wake wa miaka minne.

Aliyekuwa Mwenyekiti Simba SC, Sweddy Mkwabi ndiye aliyemchukulia fomu Wallace Karia ya kugombea tena nafasi ya Urais wa TFF kwenye uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi August mwaka huu.

Karia ambaye anamaliza muda wake kama Rais wa TFF anatarajia kugombea ili kutetea nafasi yake kwa ajili ya kuongoza kwa miaka mingine minne ijayo.

Lameck Nyambaya amechukua fomu ya kuwania nafasi ya kamati kamati ya utendaji kwenye uchaguzi Mkuu.

IMEANDIKWA NA Hamza Fumo, Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button