Tetesi za Soka Ulaya kumenoga

Winga wa Colombia Luis Diaz, 28, ameweka wazi kuwa anataka kuondoka kwa Reds baada ya klabu hiyo kukataa dau la pauni milioni 58.6 kutoka kwa Bayern Munich. (Athletic – michango inahitajika)
Leeds UnLeeds United imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 27. (Athletic- Usajili unahitajika)ited imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 27. (Athletic- Usajili unahitajika)
Tottenham inachuana na Inter Milan kumsajili beki wa Ubelgiji Koni de Winter, 23. (i paper)

Bournemouth imewasilisha dau la pauni milioni 59 kumsajili beki wa Ukraine Illia Zabaryni, 22, ambaye anasakwa na Paris St-Germain. (Independent)
Chelsea iko tayari kuanza mchujo wa msimu wa kiangazi huku mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 25, akiwa katika mazungumzo ya kurejea Benfica na Mfaransa Christopher Nkunku, 27, pia anatarajiwa kuondoka. (Standard)
Manchester United imewasilisha rasmi ombi la kumsajili kiungo wa Juventus na Mbrazil Douglas Luiz msimu huu kiangazi, huku Everton pia ikimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)

Beki wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Saudi Pro. (Mirror)
The Reds imeweka bei ya pauni milioni 43.5 kwa Konate kwa vilabu vyovyote vinavyotaka kusajili mchezaji huyo msimu huu wa kiangazi. (AS – kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa klabu ya Sassuolo na Italia, Andrea Pinamonti ananyatiwa na klavu ya Ligi ya Premia West Ham, huku wapinzani wa London Brentford pia wakiulizia kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Standard)
Leeds United ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Gonzalo Garcia, 21, kwa mkopo kutoka Real Madrid. (TBR Football)






