Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Coutinho, Willian, Higuain, Shelvey, Casilla, na wengine sokoni

Barcelona imesema iko tayari kupokea ofa ya kumnunua kiungo wao wa kati Philippe Coutinho, 26. Manchester United imeonyesha nia ya kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool katika wakati wa msimu wa joto. (Calciomercato, via Star) Barcelona pia wameweka dau la pili la kumnunua Willian ambaye ni winga wa Chelsea na Brazil, baada ya ofa yao ya kwanza ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 30 kugonga mwamba siku ya alhamisi. (Standard)

Chelsea imekubali kuwanunua kwa masharti viungo wa kati Nicolo Barella, 21, kutoka klabu ya Cagliari na Leandro Paredes, 24, wa klabu ya Zenit St Petersburg(Telegraph)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa klabu hiyo inaendelea kuzungumza na wawakilishi wa mshambuliaji Gonzalo Higuain licha ya tetesi kuwa mshambuliaji huyo huenda akahamia Chelsea. (Express)

Kumsaini kwa mkopo Higuain hadi mwisho wa msimu huu ndio mpango wake wakati huu wa uhamisho wa wachezaji. (Sun)

Baba yake Neymar ambaye ni nyota wa kamtaifa wa Brazil na Paris St-Germain amepinga uvumi kuwa nyota huyo wa miaka 26 anataka kurejea katika klabu yake ya zamani Barcelona. (Express)

Liverpool na Fulham wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Israel Moanes Dabour, 26. (Estadio Deportivo – in Spanish)

Meneja wa Everton Marco Silva amesema hana hofu hata ikiwa klabu yake haitaongeza mchezaji yeyote wakati huu ambapo dirisha la uhamisho wa wachezaji liko wazi.

Marcos hata hivyo ameongeza kuwa angelipendelea kuwasaini wachezaji “wawili watatu” wapya . (Liverpool Echo)

West Ham wanatafakari uwezekano wa kumhamishia Newcastle kiungo wake wa kati Jonjo Shelvey. (Mail)

Leeds wanajiandaa kumsaini kipa wa Real Madrid Kiko Casilla.

Kipa huyo wa miaka 3anatarajiwa kusafiri England wiki ijayo. (Yorkshire Evening Post)

Vilabu kadhaa vinavyoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A vimeonyesha azma ya kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Congo Aaron Tshibola, 24.

Tshibola amekuwa akicheza kwa mkopo katika uga wa Kilmarnock msimu huu. (Birmingham Mail)

Juventus wana mpango wa kumsaini tena Paul Pogba, 25, Manchester United endapo winga wa Brazil Douglas Costa, 28, atahamia Old Trafford kama sehemu ya mpango huo. (Tuttosport, via Calciomercato)

Juventus pia wako tayari kumuachilia beki wa kati wa Morocco Medhi Benatia, 31, kuenda Arsenal katika hatua ambayo itamwezesha Aaron Ramsey, 28, kuhamia upande wowowte. (Gazzetta dello Sport, via Metro)

Barcelona wanatafakari uwezekano wa kumchukua mshambulaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata, 26 kwa mkopo.

Morata huenda akanunuliwa na Sevilla na Atletico Madrid. (Sport – in Spanish)

Nahodha wa Arsenal Laurent Koscielny, 33, amekataa ombi la Monaco la kutaka ajiunge nao. (Le10 Sport, via Mirror)

Monaco wamezungumza na Chelsea kuhusu mpango wao wa kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25.

Agenti wake wameenda Ufaransa kujadili uwezekano huo. (Goal)

Everton wameonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Southampton na Portugal Cedric Soares, 27. (Sun, via Star)

Winga wa Hull City Jarrod Brown wa huenda akasainiwa na Leicester City huku Tottenham na Everton wakimfuatilia kiungo huyo wa miaka 22. (Sun)

Hull wanakaribia kumaliza mchakato wa kumsaini kwa mkopo mlinzi wa Cardiff City Matthew Connolly, 31. (Hull Daily Mail)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents