Tetesi za usajili barani Ulaya Lukaku kutua Inter Milan,Madrid yaanza kuhaha kuisaka saini ya Neymar

Tetesi za usajili barani Ulaya Lukaku kutua Inter Milan,Madrid yaanza kuhaha kuisaka saini ya Neymar

Real Madrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27. (Sky Sports). Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal)

Manchester United wako tayari kulipa £81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV – via Mail)

Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail)

Leroy SaneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLeroy Sane (Kulia)

Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa £8m tu. (Mirror)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipingiwa upatu kuhamia Everton. (Express)

Palace wameiambia Everton hawatakubali kupokea chini £100m kumwachilia mshambuliaji huyof. (Guardian)

Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaREUTERS

Everton wanatarajiwa kuwasajili beki waChelsea na kiungo wa kimataifa wa England wa wachezaji wa chinii ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, na beki wa kati wa Bournemouth Mholanzi Nathan Ake, 24. (Sun)

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa kulia – na nyuma Mswidi Emil Krafth, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Amiens. (Newcastle Chronicle)

Burnley wamewasilisha ombi la dakika ya mwisho kumsaini kiungo wa kati Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mail)

Danny DrinkwaterHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Tottenham wanakaribia pia kumsaini bekki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)

Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili mchezajiwa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Independent)

Kingo wa kati wa Juventus Sami Khedira, 32, amekataa uwezekano wa uhamisho mara mbili kwa sababu anaazimia kujiunga na Arsenal. (Star)

Sami KhediraHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSami Khedira, kiungo wa kati wa Juventus

Wolves wamesitisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25. (Express & Star – via Daily Echo)

Robert Lewandowski ametoa wito kwa Bayern Munich kuwasajili wachezaji watatu wapya.

Mshambuliaji huyo wa Poland anataka kuimarishwa kwa safu ya mashambulizi baada ya wachezaji nyota kuhama klabu hiyo. (Goal)

Robert LewandowskiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRobert Lewandowski
Chanzo BBC.
By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button