Michezo

Tetesi za usajili Yanga, Simba, Azam FC

Ligi Kuu soka Tanzania Bara maarufu kama NBC ipo katika hatua za lala salama,  huku Yanga SC ikijikita kileleni zaidi mwa msimamo na kuonyesha dhamira yao ya dhati ya kulitwaa kombe hilo msimu huu baada ya kulikosa kwa misimu kadhaa nyuma na hivyo wanahitaji point tatu tu za ‘jasho na damu’ kulichukuwa wakati ambapo Simba SC imeonyesha kulikosa baada ya utawala wa miaka minne wakiwa na kikosi cha dhahabu kilichoongozwa na mafundi wa mpira kama vile Clatous Chama, Luís Jose Miquissone na wengine wengi.

Imekuwa ni kawaida kwa Klabu mbalimbali za ndani na hata Barani Ulaya kuhusishwa na Tetesi za usajili kwenye kipindi kama hiki ambapo Ligi nyingi zinapofikia ukingoni katika hatua za kuboresha na kuimarisha vikosi vyao na kuviandaa vema kwa msimu unaofuata.

TETESI:

Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati, Mabingwa watetezi wa NBC, FA na Mapinduzi Cup Simba SC kwa tetesi zilizopo ni kuwa wapo katika hatua za mwisho kumaliziana na Mshambuliaji, Ceasar Lobi Manzoki ambaye ni kinara wa ufungaji katika Ligi ya Uganda kupitia klabu yake ya Vipers.

Beki wa kati fundi wa mpira, Nassoro Kapama amehusishwa kujiunga na klabu ya Simba SC. Kapama pia tetesi zinamhusisha kuwindwa na matajiri wa Dar es Salaam Azam FC.

Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara na mabingwa wapya watarajiwa kutokana na msimamo wa Ligi ya NBC, Yanga SC wamehusishwa na mchezaji Bernard Morrison.

Klabu ya Simba inahusishwa na tetesi za usajili wa straika wa timu ya Vipers ya Uganda Yunus Sentamu raia wa Uganda, msimu wa 2020/21 alipachika mabao 16 na kuwa mfungaji bora wa ligi ya hiyo.
Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents