Afya

Texas Marekani: Hakuna kuvaa barakoa, biashara zifunguliwe (+ Video)

Texas itaondoa hitaji la watu kuvalia barakoa na kuruhusu biashara kufunguliwa kikamilifu kuanzia wiki ijayo Gavana Greg Abbott ametangaza.

” Sasa wakati umewadia kuifungua Texas kwa asilimia 100′ amesema gavana huyo wa chama cha Republican .

Texas ndio jimbo kubwa la Marekani kutamatisha uhitaji wa kuvalia barakoa. Bwana Abbott amekosolewa na chama chake kuhusu uamuzi wake baada ya masharti ya kuwataka watu kuvalia maski kuwekmwa mwezi Julai mwaka jana .

Lakini utawala wa rais Joe Biden umeshikilia kwamba masharti ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona yangali yana umuhimu. Tangazo hilo la Texas limetokea huku majimbo mengine yakiwemo Michigan, Louisiana na Mississippi pia kuchukua hatua kama hiyo ya kufutilia mbali mahitaji ya watu kuvalia barakoa.

Kuanzishwa kwa chanjo ya Corona nchini humo kumezua matumaini ya hali kurejea kama ilivyokuwa kabla ya janga la corona.

Siku ya jumanne rais Biden alisema Marekani ipo mbioni kuhakikisha inapata chanjo ya kumpa kila mtu mzima nchini humo kufikia mwezi Mei . Hata hivyo msururu wa hatua za majimbo kadhaa kufungua shughuli za kawaida umezifanya serikali nyingi za majimbo kutofautiana na utawala wa Biden na maafisa wakuu wa afya ambao wametamaushwa na hali hiyo kwani wanahisi wakati huu ni hatari sana kulegezwa kwa masharti ya kupambana na virusi vya Corona .

Siku ya jumatatu mkurugenzi wa CDC alionya kuhusu ‘Awamu ya nne’ ya maambukizi ya juu iwapo nchi hiyo itafanya utepetevu katika kuzuia maambukizi ya virusi hivyo .

Kwa jumla Marekani imesajili zaidi ya maambukizi milioni 28 na vifo 516,000 vinavyohusiana na Covid 19 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Gavana wa Texas alitangaza nini?

Bwana Abbott alitoa agizo kuu la afisi yake akibatilisha maagizo makali ya kupambana na Corona aliyokuwa ametoa hapo awali wakati janga hilo liliporipotiwa .

Agizo hilo jipya linalofaa kuanza kutekelezwa Machi tarehe 10 linaondoa mahitaji yote ya kuvalia maski na linazuia maamlaka kuwaadhibu wakaazi wanaokosa kuvalia maski. Pia linaondoa vikwazo kutoka kwa biashara zilizo kwenye kaunti ambazo hazina idadi ya juu ya wagonjwa wa Covid 19 hospitalini.

Greg Abbott (file picture)

Je Covid 19 imeiathiri vipi Marekani?

Idadi ya watu milioni 28.7 walioambukizwa covid ni takriban mara dufu ya watu milioni 11 walioambukizwa nchini India inayoshikilia nafasi ya pili na Brazil (Milioni 10.5) kulingana na utafiti wa Chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Marekani ni ya tisa kwa idadi ya vifo vilivyotokana na Covid 19 kwa mujibu wa maafa yanatokea katika kila idadi ya watu 100,000 nyuma ya Uingereza na Italia.

President Joe Biden speaks about the administration's response to the coronavirus pandemic at the White House in Washington
Rais Biden amewataka Wamarekani kuwa macho dhidi ya tisho la virusi

Takriban Wamarekani 90,000 wanatarajiwa kupoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo kufikia Juni tarehe 1 utafiti uliofanywa na Institute for Health Metrics and Evaluation (IHME) umeonyesha. Kufikia mwisho wa mwezi Mei virusi hivyo vitakuwa vimesababisha maafa ya Wamarekani 500 kwa siku kutoka idadi ya sasa ya 2000 .

Idadi ya wanaolazwa hospitalini imepungua kabisa tangu mwezi Januari.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CL8-d0lB9su/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents