Michezo

TFF yaufungia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Taarifa ya leo Februari 28, 2025 iliyotolewa na TFF imebainisha kuwa miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu huku vilabu vikikumbushwa kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.

Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents