Burudani

The Fate of the Furious yavunja rekodi ya box office duniani, yaingiza $532m

Filamu ya kampuni ya Universal Pictures‘ The Fate of the Furious imevunja rekodi kwakuwa na ufunguzi mkubwa zaidi wa muda wote baada ya kuingiza dola milioni 532 kwenye majumba ya sinema duniani mwishoni mwa wiki.

Kiasi hicho ni $98.8m toka Marekani na Canada $433.2m toka nchi zingine 63 mwishoni mwa wiki. Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Star Wars: The Force Awakens iliyoingiza $529m.

The Fate of the Furious imeifanya Universal ifikishe dola bilioni 1 za makusanyo ya kimataifa ya filamu zake Ijumaa hii. Filamu hiyo imeingiza mkwanja wa kutosha kutoka Argentina, Colombia, Egypt, Estonia, India, Indonesia, Israel, Lebanon, Malaysia, Middle East, Pakistan, Panama, Paraguay, Peru, Portugal, South Africa, U.A.E., Uruguay, Venezuela, Belgium, Bolivia, Brazil, China, Denmark, Ecuador, Israel, na Mexico, Croatia, Czech Republic, Hong Kong, Iceland, Korea, Lithuania, Slovakia, Ukraine, U.K. na Ireland.

China pekee, ndani ya siku 3, filamu hiyo imeingiza $192.1m, kiasi ambacho hakijawahi kutokea nchini humo kwa filamu ya Hollywood.

Filamu hiyo imeongozwa na F. Gary Gray-na inajumuisha mastaa kama Vin Diesel, Dwayne Johnson, Michelle Rodriguez, Jason Statham, Tyrese Gibson, Chris “Ludacris” Bridges, Nathalie Emmanuel, Elsa Pataky, Kurt Russell, Scott Eastwood, Charlize Theron na Helen Mirren.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents