Fahamu

Tiger Woods alikuwa mwenyewe kwenye gari na amekutwa mzima ila ameumia miguu (+ Video)

Mchezaji maarufu wa gofu Duniani kutoka nchini Marekani @TigerWoods jana usiku amepata ajali ya gari mjini Los Angeles Jumanne, na kupelekea kupata majeraha kadhaa mwilini ambapo amelazimika kufanyiwa upasuaji. Taarifa ya Polisi wa Los Angeles imeeleza kuwa Woods ameumia zaidi kwenye miguu.

Mkuu wa polisi Alex Villanueva baadae alisema kuwa Woods ”alikuwa hai na mwenye fahamu” katika eneo la ajali.

Kamishna wa Shirikisho la mchezo wa golf Jay Monahan alisema: ” Tunasubiri taarifa zaidi atakapotoka kwenye upasuaji.

”Kwa niaba ya shirikisho na wachezaji wetu, Tiger yuko kwenye maombi yetu na tutampa ushirikiano wakati akirejea katika hali yake.”

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/tv/CLqxItUhIKM/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents