Michezo

Tigo, Parimatch, na Hisense Tanzania Wazindua Promosheni ya Kusisimua ” Zigo la Euro Cup na Hisense”

Dar es Salaam, Mei 21, 2024 – Tigo Tanzania, Kampuni namba moja Nchini Tanzania kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense Tanzania, wanatangaza kwa fahari uzinduzi wa promosheni ya Zigo la Euro Cup na Hisense.

Kampeni hii bunifu inatazamiwa kukamata msisimko wa Mashindano yajayo ya UEFA ya Kandanda ya Ulaya 2024, yanayojulikana kama Kombe la Euro, yaliyoratibiwa kufanyika nchini Ujerumani.
Huku timu 24 zikichuana katika miji 10 mwenyeji nchini Ujerumani, ikijumuisha Berlin, Munich, na Hamburg, Kombe la Euro huwa na mechi za kusisimua na nyakati zisizosahaulika kwa mashabiki kila mahali. Tigo, Hisense, na Parimatch wanachukua fursa hii kuhakikisha Watanzania wanafaidi uhondo huu

“Kombe la Euro si tukio la kimichezo tu; ni jambo la kimataifa ambalo linaunganisha mamilioni ya mashabiki wa soka duniani kote,” alisema Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa.

“Nchini Tanzania soka lina nafasi ya pekee katika mioyo ya wengi, tuliona hii ni fursa muhimu sana ya kuwasogeza wateja wetu karibu na hatua hiyo kupitia promosheni ya Zigo la Euro Cup na Hisense, kupitia promosheni hii wateja wanaweza kushiriki kwa kufanya malipo ya bili kupitia Tigo Pesa Super App, kujiongezea nafasi ya kujishindia zawadi kadha wa kadha za kuvutia.

“Kama kampuni iliyowekeza kwa dhati katika kuboresha matumizi ya kidijitali ya wateja wetu, tunafuraha kuwapa nafasi sio tu ya kufurahia Kombe la Euro bali pia kushiriki kwa njia ya maana pamoja na zawadi za kusisimua, wateja wa Tigo ambao hawatumii Tigo Pesa Super App wanahimizwa kupakua Aplikesheni ili kupata 1GB ya data BILA MALIPO, lakini pia watumiaji wanaweza pia kupata zawadi kwa kuwaelekeza marafiki na familia kujisajili kwa Super App wakati wa Kombe la Euro.” Alisema Pesha.

Parimatch Tanzania imejitolea kukuza chapa na kuwapa wateja thamani kupitia kampeni hii ya kipekee, iliyobireshwa.

“Tunafuraha kutangaza fursa ya maisha kwa wateja wetu na mashabiki wa soka wanaotaka kusafiri hadi Ujerumani na kushuhudia burudani ya moja kwa moja ya soka,” alisema Bw. Levis Paul, Mkuu wa Masoko wa Parimatch Tanzania. “Kwa kushirikiana na Tigo na Hisense tutaendesha droo za kila wiki ili kuchagua washindi saba ambao wataungana na mashabiki wengine wa soka kutoka sehemu mbalimbali duniani kushuhudia michuano ya Euro 2024 itakayofanyika Frankfurt nchini Ujerumani, promosheni hii inapatikana kwa wateja wetu wote wa zamani na wapya.”

Naye , Bi Tahera Karim, Meneja wa Hisense Tanzania, amesema “Tunafuraha kuwa sehemu ya promosheni hii ya kusisimua na Tigo na Parimatch.

Hisense imejitolea kuleta teknolojia bora zaidi ya burudani kwa wateja wetu. Kupitia promosheni hii , tunalenga kuboresha hali ya utazamaji kwa
mashabiki wa soka nchini Tanzania na kuwapa fursa ya kujishindia zawadi, zikiwemo vifaa vyetu vya kisasa vya kielektroniki.”
Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka amana kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka. ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.

“Nawahimiza Watanzania wote kuendelea kuweka pesa zao kupitia Tigo Super App na kucheza na Parimatch kupitia tovuti yetu ya www.parimatch.co.tz ili kuingia kwenye droo ya shindano hili la kusisimua,” aliongezea Paul.
Promosheni ya Zigo la Euro Cup na Hisense inaonyesha dhamira ya Tigo Tanzania katika kutoa uzoefu wa kibunifu na wa kuridhisha kwa wateja wake huku ikichangamsha matukio makubwa kama vile Kombe la Euro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents