HabariTechnology

TikTok yatozwa faini ya £12.7m kwa matumizi mabaya ya data za watoto

TikTok imetozwa faini ya £12.7m zaidi ya Tsh milioni 25 na shirika la uangalizi wa data la Uingereza kwa kushindwa kulinda faragha ya watoto.

iligunduliwa kuwa TikTok iliruhusu hadi watoto milioni 1.4 wa Uingereza wenye umri wa chini ya miaka 13 kutumia ukumbi huo mnamo 2020.

Tovuti hiyo ya kushiriki video ilitumia data ya watoto wa umri huu bila idhini ya wazazi, kulingana na uchunguzi wa Ofisi ya Kamishna wa Habari (ICO).

TikTok ilisema “imewekeza sana” kukomesha watoto wa chini ya miaka 13 kufikia programu hiyo

ICO ilisema wengi waliweza kufikia tovuti licha ya TikTok kuweka 13 kama umri wa chini wa kuunda akaunti.

Written by @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents