Technology

Tiwa Savage anatumia TECNO CAMON 20

TECNO Tanzania imezindua rasmi mfululizo wa matoleo ya Camon 20, ghafla ya uzinduzi wa matoleo hayo ulifanyika Mei 20 katika hoteli ya nyota 5 jijini Dar- es- Salaam, tayari Camon 20 premier imekuwa gumzo miongoni mwa wapenda simu janja. Mahadhi ya muonekano wake kwa nyuma na features zenye kuongeza chachu katika kuchukua video au picha katika nyakati na hali tofauti tofauti pasipo mawimbi na ukungi ni dhahiri TECNO IMEKUJA KIVYENGINE.

TECNO imezichanga vyema karata zake, imeweza kubadili muonekano mzima wa simu za TECNO na si kama ambavyo tumezizoe, teknolojia ya Magic Skin na Ceramic kuna itambulisha upya TECNO katika ulimwengu wa simu janja kuwa Kampuni nambari moja ya simu yenye kupokea mabadiliko ya teknolojia kwa haraka. 

UWEZO WAKE: Enheee, kabla sijaizungumzia Megapixel 108+50+2 za camera ya nyuma naomba kwanza TECNO ipewe Maua yake kwa ukomavu mkubwa wa kutambulisha teknolojia ya RGBW pro katika simu hii kama ilivyo kwa Samsung kuongeza uwezo wa upigaji picha ang’avu zaidi kulingana na size ya pikseli na kuonesha kilichopo kwa udogo kwa rangi yake halisi, hii imerudisha matumaini makubwa kwa wadau wa simu za TECNO.

Mabadilko mengi yamefanywa na TECNO ikiwemo muonekano wenye hadhi ya kisasa, camera kama ambavyo nimesema hapo awali lakini cha kufurahisha zaidi kampuni hii haijabadilisha utamaduni wake wa kumjali mteja wake kupitia bei. TECNO Camon 20Premier inapatikana kuanzia sh.400,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents