HabariMichezo

Tottenham yalaani ubaguzi wa rangi kwa Mathys Te kisa kukosa penati

Tottenham wamesema “wamechukizwa” na unyanyasaji wa kibaguzi aliopokea mshambuliaji Mathys Tel kufuatia kushindwa kwao na Paris St-Germain kwenye michuano ya Uefa Super Cup.

Klabu hiyo, ambayo ilishindwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kuongoza kwa mabao mawili kwa moja, ilisema watu waliotuma ujumbe wa matusi kwa Tel kwenye mitandao ya kijamii “si chochote ila waoga”.

Tel, 20, aliingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 79 na alikuwa mmoja wa wachezaji wawili wa Spurs ambao walishindwa kufunga bao kwenye mikwaju ya penalti.

“Mathys alionyesha ujasiri wa kusonga mbele , lakini wale wanaomnyanyasa si chochote ila waoga – wanaojificha nyuma ya majina ya watumiaji na wasifu ambao haukujulikana kudhihirisha maoni yao ya kuchukiza,” Tottenham ilisema.

“Tutashirikiana na mamlaka na mitandao ya kijamii kuchukua hatua kali iwezekanavyo dhidi ya mtu yeyote ambaye tunaweza kumtambua.

“Tunasimama na wewe, Mathys.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents