TRA yatoa ufafanuzi watumishi wake kushambuliwa wakidaiwa watekaji
TRA yatoa ufafanuzi wafanyakazi wake kushambuliwa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa inasikitika kuutaarifu umma kuwa gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yalioyoingia nchini kinyume na taratibu za forodha na kutolipiwa ushuru imeshambuliwa na watumishi hao kuumizwa.
TRA imesema kuwa tukio hilo limetokea eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es Salaam Desemba 5, 2024 na kwamba kadhia hiyo imetokea baada ya watumishi hao kubaini kwamba gari namba T229DHZ aina ya BMW x6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za kodi.
TRA imesema wakati watumishi wao wanatimiza wajibu walihusishwa na kitendo cha utekaji kilichosababisha wao na gari kushambuliwa.
Written by Janeth Jovin