Travis Scott aachiwa kwa dhamana
Mwanamuziki Travis Scott ameripotiwa kuachiwa huru kwa dhamana, baada ya kukamatwa siku ya jana Alhamisi asubuhi kwa kosa la ulevi kupindukia.
Kwa mujibu wa tovuti ya CNN, Travis alifanikiwa kuachiwa huru kutoka katika kituo cha polisi cha Guilford Knight baada ya kutoa dhamana ya dola 650 sawa na sh 1.5 Milioni.
BradfordCohen ambaye ni mwanasheria wa Scott aliweka wazi sababu ya msanii huyo kuwekwa kizuizini kwa muda mfupi ni kutokana na kutoelewana na watu waliyokua eneo la tukio lakini hakukuwa na shambulio lolote la majeraha ya kimwili.
Hii ni mara ya pili Travis kukamatwa na Polisi mara ya kwanza alitiwa nguvuni wakati wa onesho lake la Lollapalooza mwaka 2015 na kuhukumiwa mwaka mmoja.
Utakumbuka kuwa ndani ya wiki hii naye mwanamuziki wa Marekani Justin Timberlake aliporitiwa kukamatwa na Polisi baada ya kukutwa anaendesha gari akiwa amelewa.