HabariSiasa

Trump alimshinikiza makamu wake kubatilisha matokeo -Mashahidi

Kamati ya Bunge la Marekani inayochunguza uvamizi wa majengo ya Bunge mwaka uliopita imepokea ushahidi unaoonesha kuwa rais wa zamani Donald Trump alimshinikiza makamu wake kubadili matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Ushahidi huo umetolewa na wasaidizi wa karibu wa makamu wa rais wa zamani wa Marekani Mike Pence katika duru ya tatu ya uchunguzi wa wazi unaofanywa na Bunge la Marekani kuhusu mkasa wa kuvamiwa kwa majengo ya bunge mnamo Januari 6 mwaka jana.

Kamati inayochunguza kisa hicho imefafanua jinsi Trump alivyomtia kishindo Pence akimtaka kubadili matokeo ya uchaguzi licha ya kuarifiwa mara kadhaa kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Marc Short, aliyekuwa mkuu wa utumishi wa ofisi ya makamu wa rais amesema kupitia ushuhuda kwa njia ya video kuwa Pence alimwarifu mara nyingiTrump  kwamba haiwezekani kusitisha kura ya kumuidhinisha Joe Biden kuwa rais.

Hata hivyo inaarifiwa Trump aliendelea kumshinikiza Pence kutafuta njia za kuyakataa matokeo na ikiwezekana kutumia nafasi yake ya rais wa Baraza la Seneti kuzuia kura ya kumuidhinisha Biden. Ushahidi sawa na huo umetolewa pia na mwanasheria wa Pence, Gregory Jacob.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents