HabariSiasa

Trump alitaka kujiunga na waandamanaji katika majengo ya Bunge

Msaidizi mmoja wa zamani amesema aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump alitaka kujiunga na wavamizi wa majengo ya Bunge Januari mwaka jana.

Ufichuzi huo umetolewa na Cassidy Hutchinson, ambaye alikuwa msaidizi mwandamizi wa mkuu wa utumishi wa serikali katika Ikulu ya Marekani kwa wakati huo.

Ametoa ushahidi kuwa Trump alikasirika wakati alipoambiwa kuwa asingeweza kujiunga na wafuasi wake katika majengo ya Capitol Hill.

Pia alijaribu kuukamata usukani wa gari maalum linalombeba rais. Amesema afisa mmoja wa ulinzi alijaribu kumzuia wakati wa tukio hilo. Msaidizi huyo wa zamani wa ikulu pia alisema Trump alifahamu kuwa wafuasi wake walikuwa na silaha na kuwa wafanyakazi wake walifahamu kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu.

Ushahidi huo ni sehemu ya uchunguzi wa Baraza la Wawakilishi kuhusu vurugu zilizofanywa katika Capitol Hill Januari 6 mwaka jana. Uasi huo ulishuhudia wafuasi wa Trump wakijaribu kusimamisha kuhesabiwa rasmi kwa kura kufuatia uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka wa 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents