Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amejeruhiwa usiku wa kuamkia leo Julai 14, 2024 wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Butler, Pennsylvania.
Trump, ambaye ni mgombea urais mtarajiwa kwa tiketi ya
kutokea. Maafisa wa ulinzi wa rais kwa haraka walikimbilia kwenye jukwaa kujaribu na kumzingira kiongozi huyo huku hali ya wasiwasi ikionekana kutanda.
Damu ilionekana usoni mwake, hasa karibu na sikio la upande wa kulia. Vishindo viliendelea huku maafisa wakimhudumia jukwaani kabla ya kumshusa na kumpleka kwneye gari lililokuwa karibu.
Msafara wake uliondoka kwa haraka. Katika tarifa, ofisi ya maafisa wa ulinzi wa rais ilisema “rais wa zamani Trump yuko salama.”
Kampeni yake pia ilithibitisha kwamba yuko salama na
alikuwa akihudumiwa katika kituo cha afya.
“Ilisikika kama milio ya risasi,” mtu mmoja aliyehudhuria mkutano huo alinukuliwa na shirika la habari la Fox News
akisema.
Umati wa watu ulisiskika ukimshangilia wakati akiondolewa
kwenye jukwaa na kupelekwa kwa gari lake, huku akiinua
mkono wake kuonyesha ishra ya ushindi.
Hayo yalijiri simu moja tu kabla ya kongamano kuu la chama cha Republican lililopangwa kufanyika kuanzia Jumatau mjini
Milwauke, Wisconsin, ambapo Trump alitarajiwa kutangazwa
rasmi kama mgombea urais kuelekea kwa kuchaguzi wa
mwezi Novemba mwaka huu.
Maafisa wa usalama walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema kwamba “aliyefanya shambulizi hilo si tishio tena.”
White House ilisema kwamba Rais Joe Biden alikuwa amefahamishwa kuhusu tukio hilo.
Baadaye, Biden alishutumu shambulizi hilo na kusema
“vurugu za kisiasa hazikubaliki nchini Marekani.”