Habari

Trump azionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook kuminya taarifa zake

Trump azionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook kuminya taarifa zake

Rais wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook kwa kile alichokiita kuminya taarifa zake na za mrengo wa kihafidhina.

Akiongea na wanahabari katika ikulu ya White House, Trump amesema, “Google wamekuwa wakihadaa watu wengi, ni jambo zito sana.” Akaziongeza kuwa Twitter na Facebook, “inawapasa wawe makini, hauwezi ukawafanyia watu mambo haya…tunapokea maelfu ya malalamiko juu ya jambo hili.”

Kwa mujibu wa BBC, Trump ameitaka mitandao hiyo kuwa makini baada ya awali kuishutumu Google kwa kupindua matokeo ya taarifa pale mtumiaji wa mtandao huo anapotafuta habari kumhusu “Trump news”.

Hatahivyo, Google wamekanusha shutuma kuwa mtandao wao unaupendeleo na kusema hawafungamani na itikadi yoyote ya kisiasa,Ingawa hajabainisha ni hatua gani hasa ambazo utawala wake unapanga kuzichukua.

WASHINGTON, DC – MAY 22: U.S. President Donald Trump speaks during the Susan B. Anthony List’s 11th annual Campaign for Life Gala at the National Building Museum May 22, 2018 in Washington, DC. President Trump addressed the annual gala of the anti-abortion group and urged people to vote in the midterm election. (Photo by Alex Wong/Getty Images)

Awali mshauri wa Trump wa masuala ya uchumi, Larry Kudlow amesema utawala kwa sasa unaangalia ni namna gani wataliendea suala hilo kwa kuangalia kanuni za udhibiti.

Wachambuzi wa mambo wanasema ni vigumu kwa Trump kuthibitisha madai yake na haieleweki hasa namna gani atalishughulikia suala hilo.

Hoja iliyopo ni kuwa, hatua yoyote ya kuiubadilisha mtandao wa Google itapelekea kuvunjwa kwa katiba ya Marekani hususan uhuru wa habari, japo yawezekana hatua zikachukuliwa kibiashara zaidi.

Akitumia mtandao wake pendwa wa Twitter, Trump aliishutumu Google kwa kuzipa kipaumbele habari hasi kutoka kwenye vyombo vya habari alivyovitaja kama vya mrengo wa kushoto (waliberali).

Juma lililopita Trump pia aliishutumu mitandao ya kijamii kuwa “inabagugua moja kwa moja sauti za Republican/kihafidhina,” na kuahidi kuwa “hatokubali kuacha hilo liendelee.”

Chanzo BBC.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents