Trump, Messi & Chris Brown wapagawa na alichokifanya Kendrick Lamar

Baada ya Kendrick Lamar kuzikomba Tuzo 5 Grammy wiki iliyopita, Usiku wa kuamkia leo Februari 10,2025 alitumbuiza kwenye ‘Half Time Show ya Super Bowl’ ya 59, iliyofanyika hook New Orleans Louisiana katika Uwanja wa Caesar Super Dome.
Show Hilo ilipangiliwa kwa namna ya kutoa stori fulani, kama Kendrick alivyoahidi kwenye mahojiano aliyofanya na Apple Music siku chache kabla ya Shoo hiyo.

Kendrick alitumbuiza ngoma zake kama Squable Up, Humble, TV Off, Not like Us, All Stars na nyingine nyingi. lakini pia shoo Hiyo ilichukua nafasi ya kipekee kwani aliamua kumtumia Muigizaji Samuel Jackson ‘Anko Sam’ kama Host anayempa Link za kutoka kwenye wimbo mmoja kwenda mwingine.

Hata hivyo shoo hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Donald Trump na amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhudhuria mashindano hayo. Mbali na Trump pia alikuwepo Jay Z na familia yake na mwanasoka Lionel Meddi na Mastaa wengine.

Aidha ubora wa shoo aliyofanya Kendrick umemfanya mwanamuziki Chris Brown kushindwa kuzuia hisia zake. Muda muchachee baada ya Kendrick kushuka kwenye Jukwaa Chris aliachia Ujumbe kwenye Instagram Story yake akisema, “Wow Dot” na Kisha kuweka Emoji ya moto akionesha kukubali alichokifanya rapa huyo wa Campton California. Super Bowl ambayo ipo chini ya Apple Music ni show Fupi ambayo hufanywa kwa takribani dakika 13 za muda wa mapumziko kwenye fainali za mashindano ya mchezo huy kila mwaka.

Mashindano hayo huyoa nafasi kwa wasanii kuwa kinara kwa mwaka husika ambapo 2025, Kendrick iliangukia mikononi mwake.






