Siasa

Trump: Pongezi Nigeria kuifungia Twitter, najutia sikuifungia nikiwa Rais

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepongeza hatu ya Nigeria kuipiga marufuku Twitter – na kutoa wito nchi zingine zifuate mkondo huo. “Pongezi kwa nchi ya Nigeria, kwa kuifungia Twitter kwasababu ya kumpiga marufuki Rais wao,” alisema katika taarifa.

Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi zingine kufuata mkondo na kuzifungia Facebook na Twitter ” kwa kudhibiti uhuru wa kujieleza”. Bw. Trump alipigwa marufuku na katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook mwezi Januari kwa tuhuma za kuchapisha ujumbe wa kuchochea uvamizi wa bunge la Marekani. Watu watano walifariki kutokana na kisa hicho.

Twitter

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, akijutia kwanini hakuzifungia Facebook na Twitter wakati wa Urais wake. “Wao ni nani kuamua kizuri na kibaya ikiwa wao wenyewe ni wabaya? Nadhani ningeliwapiga marufuku nilipokuwa Rais. Lakini [Mwanzilishi wa Facebook Mark] Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri,” alisema.

Wiki iliyopita Nigeria ilifunga akaunti za Twitter nchini humo kwa madai kwamba “shughuli za mtandao huo zinahujumu uwepo wa Nigeria kama taifa lililoundwa shirikisho”. Hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.

Ilizua ghadhabu miongoni mwa Wanaigeria na mataifa ya magharibi ambayo yalisema hatua hiyo inaminya uhuru wa kidemokrasi. Pande zote mbili zimesema zinajadiliana kuhusu namna ya kusuluhishi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents