Habari

Tuki-‘stop’ bodaboda tutapunguza ajali asilimia 70 – MOI

Usafiri maarufu, pendwa na wa haraka, bodaboda unatajwa kama chanzo cha  kuchangia ajali kwa asilimia 70 zinazotokea nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa naMkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dk. Respicious Boniface, katika kongamano la tatu la kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambuliza Jijini Arusha

Dk. Boniface amebainisha kuwa kati ya majeruhi 600 wa ajali kwa mwezi asilimia 70 wanatokana na ajali za bodaboda.

Dk. Boniface anafafanua kuwa japo bodaboda ni sehemu ya ajira lakini bado ni tatizo na endapo kama zikisimamishwa (kutofanya kazi) basi kiwango cha ajali kitapungua kwa asilimia kubwa jambo ambalo amesema analiachia mamlaka kulitazama kwa kina.

Mbali na taarifa hiyo Dk. Boniface anasema bado kuna changamoto za usafirishaji wa majeruhi hali inayopelekea majeruhi wengi wa ajali kutofika hospitali na wengine kuishia kufariki njiani, hali ambayo ameitaka serikali kuhakikisha inafanikisha upatikanaji wa magari ya wagonjwa ya kutosha.

Pamoja na hayo, Daktari huyo amesisitiza hospitali za Mikoa na Wilaya zinapaswa kuboreshwa kwenye majengo na vifaa ili kuweza kusaidia wagonjwa wa dharura na wale wanaohitaji uangalizi wa juu pindi anapotokea majeruhi wa ajali aweze kusaidika mapema.

Hata hivyo ameliomba Jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma ya kwanza,  pamoja kuwapatia vifaa vya huduma hiyo ili kuweza kusaidia majeruhi wanapotokea katika maeneo yao.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents