Michezo

Tunajua mna maumivu ya msiba lakini mmekuja muda mbaya – Simba SC

Mabingwa watetezi wa Michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Simba SC hapo jana iliibuka na ushindi mnono wa jumla ya magoli 7 – 0 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliyopigwa Februari 16, 2022 katika Uwanja wa Mkapa.
Baada ya ushindi huo mnono Simba SC iliposti ujumbe unaosomeka kuwa wanafahamu wapinzani wao Ruvu Shooting wanamaumivu ya msiba kwa kuondokewa na beki wao, Ally Mtoni Sonso aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita lakini kwakuwa wamekuja katika kipindi kibaya cha kucheza na wao basi ndiyo imetokea kuchezea kichapo hiko kitakatifu.  ”Tunajua mna maumivu ya msiba lakini mmekuja muda mbaya.”
Magoli matatu kwenye mchezo huo yalifungwa Mwamba wa Lusaka Triple C, Chama, mawili yakifungwa na Nahodha John Bocco, Jimmyson moja na lingine wakijifunga wenyewe.
Hii ni mara ya pili kwa Simba SC kuwafunga Ruvu Shooting kwa idadi hiyo ya magoli 7 – 0, kwani Historia inaonesha mwaka August 26, 2017 Simba ilishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Ligi Kuu Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button