Tundu Lissu afanyiwa upasuaji kwa mara ya 25, aeleza haya

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amefanyiwa upasuaji wa 25, baada ya shambulio dhidi yake mnapo tarehe 7 mwezi Septemba mwaka 2017. Tundu Lissu amechapisha katika mtandao wa twitter picha yake akiwa katika kitanda cha hospitalini na kuandika.

”Leo nimefanyiwa upasuaji wa 25 baada ya jaribio la mauaji ya Septemba 7 mwaka 2017.

Mwezi Aprili,msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania David Misime alisema uchunguzi juu kesi ya Bwana Lissu ulisimamishwa baada ya kukataa kujibu ombi la polisi la ushirikiano katika uchunguzi huo .

Aidha Bw Misime alisema polisi wana wajibu wa kisheria wa kuwalinda watu na mali zao bila kujali utaifa wao, kutambua, kuzuia na kutekeleza sheria ili kuimarisha Amani, na usalama na mwingiliano.

Alisema polisi wanahakikisha usalama kwa raia wote bila ubaguzi na upendeleo, akisema changamoto za kiuslama zinapaswa kuripotiwa kulingana na taratibu ili mamlaka husika zichukue hatua.

Mara baada ya shambulio dhidi yake tarehe 7 Septemba, 2017, Bw Lissu alisafirishwa kwa ndege hadi katika Hospitali ya Nairobi Kenya ambako alipokea matibabu kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu maalumu.

Related Articles

Back to top button