Uncategorized

TuneCore: Fursa nyingine kwa wasanii Bongo

Kampuni ya muziki kutoka New York nchini Marekani, TuneCore, imeijumuisha Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi saba za Afrika ambazo wasanii wake watapata huduma yao inayotajwa kuwa na maslai makubwa.

 

 

 

Nchi nyingine ni Nigeria, Ghana, Gambia, Liberia, Ethiopia na Sierra Leone ambapo wasanii wake watapata huduma ya kusambaziwa muziki wao duniani kote na kupata malipo ya uhakika.

Mwakilishi wa TuneCore kwa nchi za Afrika Magharibi na Mashariki, Chioma Onuchukwu kutokea Nigeria amesema TuneCore inajivunia kuwa na uwezo wa kulipa wasanii waliochini yao asilimia 100 ya mirahaba yao.

“Tunasambaza muziki wa msanii moja kwa moja kwa wateja zaidi Milioni 150 kwenye nchi 200 bila kuwapo kwa madalali kwenye biashara hii, huku msanii akiendelea kumiliki muziki wake kwa asilimia 100, na kila mara tunatoa ripoti ya biashara yake kwa wazi bila kuficha chochote,” amesema Onuchukwu.

TuneCore pia inafanikisha huduma ya usimamizi ya malipo kwa wasanii kwenye mitandao (monetization) ya YouTube, Facebook na Instagram kwa urahisi zaidi.

Amesema ni wakati wa muziki wa Kiafrika kwenda ulimwenguni kote na kutamba na kuongezeka kwa wasanii wenye uhuru wa kiuchumi kila siku wanapofanya mambo makubwa kwenye tasnia.

TuneCore watahakikisha wasanii wanapata kila dola wanayotengeneza, inayojulikana na isiyojulikana.

“Tuna timu dhabiti inayoshughulikia na kusaidia wasanii wa Kiafrika katika mchakato wa usambazaji muziki wao kupitia blog yetu ambayo ina vifaa vya kisasa, vidokezo na miongozoya kumsimamia msanii kuanzia kuzalisha, kusambaza na kutangaza muziki wake,” anasema Onuchukwu.

Anasema kutokana TuneCore ni jukwaa la usambazaji la DIY, hawasaini mkataba na msanii yeyote wala kushawishi kufanya hivyo kwa kuwa hawataki kuathiri au kuwa na udhibiti wowote juu ya uhuru wa ubunifu wa msanii husika.

Mwisho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents