Tupo tayari – Simba SC

Mabingwa wa Nchi na Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati Simba SC hii leo wanatarajia kushuka uwanjani kukabiliana na Jwaneng Galaxy katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika CAF utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa wa Botswana.

Simba wamejinasibu kuwa wapo tayari kuzipigania alama tatu muhimu huku wakiwaheshimu wenyeji wa mchezo huo klabu ya Jwaneng Galaxy.

“Namna bora ya kuwa na mchezo mzuri ni kumheshimu mpinzani. Itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga vizuri sana na kwa nilichokiona leo mazoeni tutakuwa na mchezo mzuri.”- Kocha Mkuu Didier Gomes Da Rosa.

Kwa upande wake beki wa klabu hiyo Shomari Kapombe amesema kuwa wachezaji wapo tayari asilimia 100 “Kila mchezaji yuko tayari kwa asilimia 100% kuipigania Simba kwenye mchezo wa kesho.”

Mchezo wa Jwaneng Galaxy dhidi ya Mnyama Simba SC unatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni kwa Tanzania wakati kwa Botswana ikiwa ni saa 9:00 alasiri.

Related Articles

Back to top button