Tutaendelea na tozo : Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kwamba Tanzania itaendelea na suala la Tozo kwani ni sehemu mojawapo ya nchi kujiimarisha kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 15, katika Viwanja vya Ushirika vilivyopo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na wananchi kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani huko.

“Udume wa Mwanaume ni kujitegemea na uimara wa Nchi ni kujitegemea, tumeanzisha tozo hizi ambazo kwa kipindi cha miezi mitatu vituo vya afya 200 vinajengwa na madarasa 500 yanajengwa hii ni kabla ya hizi fedha za IMF (Tril 1.3) hazijafika,” Rais Samia.

Ameongeza “Niwaambie kwamba hizi fedha zilizokuja kwa mkupuo ni bahati na uhusiano mzuri na tulikoziomba na kuzikopa, lakini kama nchi lazima tuwe na chanzo chetu na chanzo cha elimu na afya ni hizi tozo, zilipigiwa kelele sana”

Mbali na Tozo pia Rais amewashukuru wananchi wa Kilimanjaro kuurudisha mkoa huo kuwa chini ya Chama cha mapinduzi baada ya muda mrefu kuongozwa na vyama vya upinzani vikiwepo CHADEMA na NCCR Mageuzi.

Nawashukuru kwa kazi nzuri mliyoifanya Oktoba 2020, mlituthibitishia kwamba ile likizo mliyoitoa kwa imeisha na mkasema sasa tunataka maendeleo, na kwa maana hiyo mkairudisha CCM madarakani ile ilikuwa kazi nzuri sana“- Rais Samia

Akizungumzia suala la Moshi kuwa Jiji na Vunjo kuwa Halmashauri , Rais Samia amesemakwamba inabidi tuangalie vizuri.

“Moshi inataka kuwa Jiji, ila kutoka Moshi-Vunjo ni KM 20 au 25 pia kuna suala la vigezo tukiangalia Moshi haijafikia ila tutaangalia kuvunja Vunjo iiingie ndani ya Jiji au vinginevyo” Rais Samia.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button