HabariMichezo

Tutawauliza Singida Big Stars ile sare waliipataje- Ahmed Ally

Kikosi cha Simba SC kimetangaza kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Ijumaa saa moja usiku.

Baada ya mchezo wa hatua ya tatu ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Coastal Union juzi wachezaji wa Simba SC walikuwa wakifanya mazoezi kwa kutokea nyumbani.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri “Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Liti tulitoka sare sasa tunataka kuwauliza ile sare waliipataje,” amesema Ahmed.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents