
Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amewataka mashabiki wa timu hiyo watulie na kuwa na imani na viongozi wao.
Dewji ambaye pia ni Muwekezaji ndani ya Klabu hiyo ameongeza kwa kuwahamasisha mashabiki kuendelea kufika Uwanjani kuishabikia timu yao.
Hayo yanajiri baada ya kupita wiki ‘NGUMU’ yenye majuto kwa Mnyama kutokana na kuchezea kichapo cha ‘AIBU’ cha goli 5-1 kutoka kwa Yanga SC.
Simba kufungwa goli tano sio jambo kubwa ila je, hizo 5 kafungwa na nani hicho ndicho kilichomtesa Mnyama kwa zaidi ya wiki na mashabiki wake kuchafua hali ya hewa wakiwataka viongozi kuchukua hatua kama ilivyokuwa kwa Kocha Robertinho.