Tuzo za Watu 2015: Ukweli kujulikana leo usiku, Hyatt Regency Hotel

Baada ya wiki kadhaa za mpambano mkali wa kura za tuzo za watu, leo ndio fainali.
Majina matatu yanashindania tuzo kwenye vipengele 13 vya mwaka huu. Majina hayo yameingia baada ya kuvuka michujo miwili migumu. Ni kura za mashabiki peke yake ndio ziliwaingiza kwenye fainali hiyo na mshindi atapatikana kwa kura za wananchi, hakuna kingine.
Washereheshaji kwenye fainali hizo ni Vj Penny na mchekeshaji Dogo Pepe huku muimbaji wa kike anayechipukia kwa kasi Ruby akitarajiwa kutumbuiza.
“Watu wategemee performance nzuri kutoka kwangu,” amesema Ruby. “Kama kawaida mimi napenda muziki mzuri na itakuwa ni live performance. So wategemee kizuri na hali ya hewa ya muziki na yenyewe itabadilikabadilika kutoka kwa Ruby.”
“It’s finally here. The 2nd annual Tanzanian People’s Choice Awards,” ameandika Mwenyekiti Mtendaji wa Bongo5 Music Group, Luca Neghesti kwenye Instagram.
“Wananchi wamepiga kura kwa wingi na washindi wenye kura nyingi zaidi wamepatikana, kazi iliyobaki ni kujua majina yao na kuwakabidhi tuzo leo usiku. Hongera nyingi sana kwa nominees wote, kupendekezwa na kufika hatua ya kupigiwa kura ina maanisha kwamba mnakubalika na jamii!!! #tzw2015 #TuzoZaWatu Raha.com watawezesha show kuonekana live kupitia bongo5.com,” ameongeza.
Haya ndio majina yaliyoingia kwenye fainali
Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM
Maryam Kitosi – Times FM
Millard Ayo – Clouds FM
Kipindi cha redio kinachopendwa
Amplifaya – Clouds FM
Hatua Tatu – Times FM
Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Abdallah ‘Dullah’ Ambua – EATV
Salama Jabir – EATV/Maisha Magic
Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa
In My Shoes – EATV
Mkasi – EATV
Planet Bongo – EATV
Blog/Website inayopendwa
Hassbabytz.com
Millardayo.com
timesfm.co.tz
Muongozaji wa video anayependwa
Adam Juma
Hanscana
Nisher
Muongozaji wa filamu anayependwa
JB
Leah Mwendamsoke
Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Jacqueline Wolper
Riyama Ally
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
JB
King Majuto
Mwanamuziki wa kike anayependwa TZW10
Lady Jaydee
Linah
Vanessa Mdee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Barnaba
Diamond Platnumz
Filamu inayopendwa
Chausiku
Kigodoro
Madam
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz
Wahalade – Barnaba
XO – Joh Makini