Twitter haitaki masihara, Wafahamu watu maarufu waliofungiwa na twitter kwa kukiuka sheria zake

Mtandao wa Twitter umemfungia mwandishi maarufu wa vitabu nchini Marekani, Dkt. Naomi Wolf baada ya kusambaza taarifa potofu kuhusu chanjo ya corona.

Dkt. Wolf, ambaye ameendelea kugonga vichwa vya habari nchini Marekani kwa kitabu chake ambacho kinakosoa masuala mengi kuhusu chanjo ya corona kinachoitwa ‘The Beauty Myth’.

Akitumia mtandao wake huo wa Twitter wenye wafuasi zaidi ya 140,000, Mwandishi huyo amemfananisha pia Dkt. Anthony Fauci, mmoja wa washauri wa juu wa masuala ya Covid nchini Marekani na shetani.

Hivi karibuni pia aliweka pia kwenye ukurasa wake wa Twitter mkojo na kinyesi cha watu waliochanjwa chanjo ya corona akieleza utenganishwe na watu wasiochanjwa.

Dkt. Wolf ni mmoja tu kati ya watu mashuhuri ambao walifungiwa mitandao yao kutokana na kuchapisha taarifa potofu.

Je ni watu gani wengine maarufu waliokumbwa na rungu la kufungiwa akaunti zao?

Donald Trump

trump

Rais wa zamani wa Marekani, Donad Trump anafahamika zaidi kwa kuchapisha taarifa tata hasa wakati akiwa Rais wa nchi hiyo.

Ni miongoni mwa watu mashuhuru ambao walipenda sana kutumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 88, lakini utata wa machapisho yake yalifanya mtandao wa Twitter kumfungia na kmchunguza.

Alichapisha taarifa iliyodaiwa kuleta uchochezi, kufuatia kupinga kwake matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani, yaliyompa ushindi, Joe Biden.

Katika moja ya ujumbe wake aliandika: “Wamarekani 75,000,000 Wazalendo walionipigia kura, Marekani Kwanza, fanya Marekani kuwa bora tena, watakuwa na sauti inayosikika siku zijazo. Hawatakosewa heshima au kuchukuliwa kwa uonevu kwa namna yoyote ile!!!”.

Mtandao wa Twitter ulisema ujumbe huo “unatafsiriwa kama ishara zaidi ya kuwa Rais Trump hana mpango wa kuhakikisha kunafanyika ‘mabadilishano ya madaraka kwa njia ya amani'”.

Katika ujumbe mwingine rais aliandika: “Kwa wote ambao wameuliza, sitahudhuria hafla ya kuapishwa Januari 20.”

Mohammadu Buhari

COLLAGE

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari na yeye hivi karibuni amekutana na rungu la Twitter la kuondoa baadhi ya machapisho yake na kushikilia akaunti yake kwa kile kinachodaiwa kuchapisha taarifa zinazochochea vurugu hasa Kusini Mashariki wa nchi hiyo.

Moja ya chapisho la Rais Buhari, lililopigiwa kelele ni lile alilowasema raia wa eneo hilo la Kusini Mashariki mwa Nigeria kwa kushambulia na kuharibu miundo mbinu ya serikali.

nbc

“Wengi wa wanaofanya vitendo hivi hawaelewi kabisa kuhusu athari na vifo vilivyotokea wakati wa mapigano ya weyewe kwa wenyewe. Wengi tuliokuwa eneo la tukio kwa miezi 30 na kupigana vita, tutazungumza nao katika lugha abayo wataielewa,” alisema Buhari kwenye mtandao huo.

Raia wengi wa Nigeria walitoa taarifa Twitter, wakitaka chapisho hili liondolewe wakiliona kama linatishia na kuashiria vita.

t

Baada ya Twitter kuchukua hatua, serikali ya nchi hiyo nayo ikajibu mapigo kwa kuzuia shughuli za Twitter nchini humo.

Inaelezwa kwamba nchi hiyo ina watumiaji zaidi ya milioni 39 wa Twitter ambao wengi wao sasa baada ya mtandao huo kuzimwa nchini Nigeria wameanza kutumia njia ya VPN ili kuupata mtandao huo.

Rocker Courtney Love

Mwimbaji huyu mkongwe wa Marekani, alikuwa msanii wa mwanzoni kabisa kushitakiwa baada ya kuweka chapisho linalomdhihaki mmoja wa wanamitindo nchini humo.

Ingawa kesi hiyo iliisha juu kwa juu, lakini akaunti yake ya Twitter, iliyokuwa na wafuasi zaidi ya 620,000 ilifungiwa.

Hata hivyo Msanii huyo amefungua akaunti nyingine ya mtandao huo.

Azealia Banks

Rapa mwanadada Azealia Banks pia wa Marekani mara kadhaa na yeye alifungiwa akaunti yake kwa sababu ya kutoa maneno ya kashfa kwa wapinzani wake, akiwemo nyota Zayn Malik wa Kampuni ya One Director.

m

Steve Bannon

Mbali na hao pia afisa wa ngazi ya Ikulu ya Marekani chini ya utawala wa Trump Steve Bannon, alifungiwa akaunti yake na Twitter siku mbili baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 baada ya kumdhihaki Dkt. Anthony Fauci a mkurugenzi wa FBI Christopher Wray.

 

Abhijeet Bhattacharya

Msanii maarufu wa India, mwaka 2017 alichapisha chapisho lililomdhihaki mwanaharakati wa nchi hiyo Shehla Rashid na kusababisha Twitter kuungia akaunti yake kama ilivyotokea kwa Kamaal Rashid Khad, ambaye ni muigizaji aliyefungiwa akaunti yake mwaka huo huo.

Baada ya akaunti yake kufungiwa Kamaal alitangaza kuifungulia mashataka Twitter, baadae akafungua akaunti nyingine.

Mtangazaji maarufu wa marekani Anthony Cumia, Mwanamuziki Talib Kweli, na mwandishi maarufu na mwanaharakati nchini Misri, Wael Abbas, ni miongoni mwa watu maarufu waliokutwa na dhahma ya kufungukiwa akaunti zao na Twitter.

Hata chombo cha habari cha Aljazeera, idhaa ya kiarabu nayo ilifungiwa akaunti yake bila kuelezwa wazi sababu zake.

Mtandao wa Twitter una mamlaka ya kufungia watumiaji wake wanaokiuka masharti yaliyoweka, wakifungia kwa namna mbili; kwa muda ama moja kwa moja.

Kampeni ya kufungia akaunti zinazokiuka masharti ikiwemo ya kutochochea, ilianza mwaka 2015 na siku moja tu baada ya kampeni hiyo kuanza akaunti zaidi ya 10,000 zilifungiwa.

Credit by bbc.

Related Articles

Back to top button