HabariTechnology

Twitter yawafungia wafanyakazi nje ya ofisi hadi wiki ijayo

Twitter imewaambia wafanyakazi wake kwamba majengo ya ofisi ya kampuni hiyo yatafungwa kwa muda, na zoezi hilo kuanza mara moja.

Katika ujumbe ulioonekana na wafanyakazi waliambiwa kuwa ofisi hizo zitafunguliwa tena Jumatatu tarehe 21 Novemba. Haikutoa sababu ya zoezi hilo.

Tangazo hilo linakuja huku kukiwa na ripoti kwamba idadi kubwa ya wafanyakazi walikuwa wakiacha kazi baada ya mmiliki mpya Elon Musk kuwataka wajisajili kwa “saa nyingi kwa nguvu nyingi” au waondoke. Ujumbe huo uliendelea kusema:

“Tafadhali endelea kuzingatia sera ya kampuni kwa kuacha kujadili taarifa za siri za kampuni kwenye mitandao ya kijamii, na waandishi wa habari au mahali pengine.” taarifa hiyo ilisema.

Twitter haikujibu mara moja ombi la maoni kutoka kwa BBC.

Wiki hii Bw Musk aliwaambia wafanyakazi wa Twitter kwamba walipaswa kujitolea kufanya kazi kwa muda mrefu, kulingana na ripoti.

Katika barua pepe kwa wafanyikazi, mmiliki mpya wa kampuni alisema wafanyikazi wanapaswa kukubaliana na ahadi hiyo ikiwa wanataka kusalia, liliripoti Washington Post.

Wale ambao hawakujiandikisha kufikia Alhamisi 17 Novemba watapewa malipo ya kuachishwa kazi kwa miezi mitatu, Bw Musk alisema.

Mapema mwezi huu kampuni hiyo ilisema kuwa ilikuwa ikipunguza karibu 50% ya wafanyikazi wake. Tangazo la leo kwamba Twitter ilifunga afisi zake kwa muda lilitolewa huku kukiwa na dalili kwamba idadi kubwa ya wafanyikazi pia wamejiuzulu kwa vile hawajakubali masharti mapya ya Bw Musk.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents