Habari

Twitter yazifunga zaidi ya akaunti 3,000 kutoka nchi 6, mbili za Afrika Mashariki 

Twitter  hapo jana siku ya Alhamisi imesema kuwa imeondoa akaunti 3,465 zinazofanya kazi kama “operesheni za habari zinazoungwa mkono na serikali” ambazo ilizihusisha na nchi sita: Uchina, Mexico, Urusi, Tanzania, Uganda na Venezuela.

Nchini Uganda, Twitter iliondoa mtandao wa akaunti 418 “zilizokuwa zikishiriki katika shughuli zisizo halali” za kumuunga mkono Rais Yoweri Museveni na chama chake, National Resistance Movement.

Takriban akaunti 268 pia zilifungwa nchini Tanzania baada ya kupatikana kuwasilisha ripoti za nia mbaya kwenye Twitter.

  • Mexico – 276 akaunti
  • China – 2,160 akaunti
  • Urusi – 66 akaunti
  • Tanzania – 268 akaunti
  • Uganda – 418 akaunti
  • Venezuela – 277 akaunti

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents