Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Uchambuzi: Alikiba ameonyesha Ufalme wake, Ayra Starr ameondoka na somo kuimba live Jukwaani

Kupitia kipindi cha RECAP na MANDO @el_mando_tz amefannya uchambuzi wa Show ya Alikiba aliyoifanya pamoja na Ayra Starr siku ya Jumamosi hii katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar Es Salaam.

@el_mando_tz amezungumzia vitu kadhaa ikiwemo mpangilio wa ndani ya ukumbi ulivyokuwa lakini kubwa zaidi kuhusu show yenyewe ambayo ilikuwa ya wasanii wawili tu.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao ni alama kubwa sana kwenye muziki wa Bongo Fleva linapokuja suala la kuimba live.

@el_mando_tz ameonngeza kuwa kitu alichokifannya Alikiba wikiendi hii ni alama tosha kuonyesha kuwa kuimba live inabaki kuwa kitu muhimu kitakachomfanya msanii apenndwe jukwaani.

“Siku zote mashabiki wanapolipia kiingilio kwenye show yako huwa wanatarajia kitu special kwa sababu kama ni muziki huwa wannausikiliza kwenye radio na hata video wanaziona mitandaoni, unapoandaa show lazima uwe nna kitu cha kitofauti cha kufanya jukwaani”

Alichokifanya Alikiba nndio kitu ambacho kinamtofautisha yeye na wasanii wengine ambao likija suala la kuimba live huwa ni kitendawili kwao.

@el_mando_tz amemaliza na sababu zinazowafanya wasanii wasiimbe live jukwaani.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents