Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzFahamuHabari

UCHAMBUZI: Diamond amejiunga na Yanga kibiashara ila sio kiushabiki

Leo kama unavyojua ni siku ya RECAP & Mando, moja ya kipindi bora kabisa kwa sasa kwa upande wa burudai nchini, na @el_mando_tz amezungumzia tukio lililotokea siku ya jana pale makao makuu ya klabu ya Yanga Jangwani.

Kwa mara ya kwanza msannii na CEO wa lebo ya WCB Diamond Platnumz alitoa burudani wakati wa Parade ya Yanga ya kusherehekea mataji yao waliyofanikiwa kutwaa msimu huu ambayo ni matatu.

  1. Kombe la ligi kuu Tanzania bra NBC
  2. FA
  3. Ngamo ya Jamii

Diamond baada ya kutangaza kujiunga na klabbu hiyo akiwa kama shabiki jana alipewa nafasi ya kukutana na wachezaji wa Yanga lakini pia kutoa burudani, mbali na hilo alieleza sababu za yeye kujiunga an Yanga.

Ameeleza kuwa Haji Manara ndio amemshawishi kujiunga na Yanga lakini @el_mando_tz yeye anasema kuwa:-

Diamond amejiunga na Yanga kibiashara zaidi, annaongeza kuwa Diamonnd ameenda nna upepo wa Yanga kufanya vizuri na hata nyuma aliwahi hadi kuwatungia Simba wimbo na kutoa burudani Simba day.

Diamond ni mmoja ya wasanii wenye akili za kibiashara, alichoangalia yeye ni timu gani inafanya vizuri anna anaweza kufanya nao kazi akaona ni Yanga lakini ipo siku Simba wakiannza kufanya vizuri tena tusishangae kumuona Diamond amerudi Simba.

Je akirudi Simba mashabiki wa Simba mtampokea au mtamkataa??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents