Michezo

Uchambuzi: Simba Vs JKT Tanzania Ligi Kuu (+Video)

Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mzunguko wa 22 pale Mabingwa wa Nchi Simba SC watakapowakaribisha JKT Tanzania ya Dodoma majira ya Saa 1:00 usiku.

Mnyana Simba akiwa wamoto kweli kweli baada ya kumpiga Bingwa wa Afrika klabu ya Al Ahly 1-0, kisha kumchezshea kichapo ca magoli 3 – 0  African Lyon anakutana na JKT Tanzania akiwa hajapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo yake mitano (5) ya mwisho ya Ligi Kuu wakiwa wameshinda minne na sare moja pekee.

Mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizi zilipokutana mchezo ambao ulichezwa jijini Dodoma katika Dimba la Jamhuri Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere akifunga mawili, Chris Mugalu na Luiz Miquissone. @abbas_pira anaamini  JKT Tanzania wanatakiwa kujipanga kweli kweli kama kweli wanataka kuifunga Simba hii

Tutegemee matokeo ya namna gani usiku wa leo #simbasc Vs #kagerasugar ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents