Habari

Uchunguzi wa shambulio la Septemba 11 sasa hadharani 

Shirika la Ujasusi wa Ndani la Marekani (FBI) limeweka hadharani nyaraka za uchunguzi wa mashambulizi ya Septemba 11 na juu ya tuhuma za msaada wa Saudi Arabia kwa washambuliaji kufuatia amri ya Rais Joe Biden.

Jamaa wa wahanga wa mashambulizi hayo walikuwa wamemtaka Rais Biden kutohudhuria mikusanyiko ya kumbukumbu ya miaka 20 iliyofanyika siku ya Jumamosi (Septemba 11), endapo hakuziweka hadharani nyaraka ambazo wanaamini zingelionesha kwamba mamlaka nchini Saudi Arabia zilisaidia hujuma hiyo kutendeka.

Sehemu ya waraka huo wenye kurasa 16 iliyotolewa siku ya Jumapili (Septemba 12) inabanisha mawasiliano baina ya watekaji nyara na washirika wao wa Kisaudi, lakini ndani yake hamuna ushahidi wowote kwamba serikali mjini Riadh ilihusika na mashambulizi hayo yaliyouwa takribani watu 3,000.

Kwa muda mrefu, Saudi Arabia imekuwa ikisema kwamba haihusiki kwa namna yoyote na mashambulizi hayo.

Ubalozi wa nchi hiyo jijini Washington haukujibu ombi la kuzungumzia uwekwaji huo hadharani wa nyaraka za siri za uchunguzi wa kijasusi, lakini kwenye taarifa yake ya tarehe 8 Septemba, ubalozi huo ulisema Saudi Arabia daima imepigania uwazi kwenye matukio yanayohusiana na tarehe 11 Septemba 2001 na inafurahia hatua ya kutolewa kwa nyaraka hizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents