
Kesho, Novemba 23, itakuwa siku ya mapumziko nchini Saudi Arabia, ufalme huo ulitangaza Jumanne, katika kusherehekea ushindi wake wa kihistoria katika Kombe la Dunia la Fifa.
Inatumika kwa wafanyikazi wote katika sekta ya umma na ya kibinafsi, pamoja na wanafunzi wote kote nchini.
Saudi Arabia iliilaza Argentina wanaotabiriwa kuwa mabingwa kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Lusail mjini Doha Jumanne katika moja ya michezo mikubwa zaidi ya Kombe la Dunia katika historia.
Hii si mara ya kwanza kwa likizo ya umma kutangazwa baada ya ushindi wa Kombe la Dunia.