Bongo5 ExclusivesHabariMahojiano
Ufanisi wa Bandari ya Mtwara waongezeka
Kufuatia maboresho yaliyofanyika kwenye Bandari ya Mtwara , meli kubwa za mizigo zimefanikiwa kutia nanga kwenye bandari Hiyo na kuondoka na Shehena ya Tani elfu 80 ya korosho pamoja Kuleta viuatifu kwaajili ya zao Hilo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Norbert Kalembwe amesema ufanisi wa Bandari ya Mtwara umeongezeka zaidi Baada ya Serikali kufanya maboresho yakiwemo kuongeza gati ya nyongeza yenye kina cha Mita 300.