Ufaransa kuilipia Sudan madeni yake kwa IMF

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire, amesema kwamba nchi yake itaikopesha Sudan dola bilioni 1.5 ili kuisaidia nchi hiyo ya Afrika kulipa madeni yake makubwa katika Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, mnamo wakati nchi hiyo inajaribu kuinuka baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu.

Macron says agreement in place to cancel Sudan's $5 billion French debt

Le Maire amesema Rais Macron mwenyewe atathibitisha msaada huo baadaye leo. Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa unaolenga pia kuisaidia Sudan kurudi katika njia ya kidemokrasia.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock anahudhuria mkutano huo mjini Paris, akitafuta msaada wa kulipa mzigo wa deni la dola bilioni 60, lakini pia akilenga kutafuta mikataba ya uwekezaji.

Hamdock anajaribu kuijenga upya Sudan, kuleta mageuzi katika uchumi uliodhoofika wa nchi hiyo na kumaliza hatua ya Sudan kutengwa na jumuiya ya kimataifa kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa dikteta Omar al-Bashir, ambaye utawala wake wa miongo mitatu ilisababisha hali ngumu kiuchumi kwa taifa hilo na pia vikwazo vya kimataifa.

Related Articles

Back to top button