Habari

Ufaransa yaingilia kati mzozo wa Tunisia

Ufaransa imeisihi Tunisia kuteua haraka Waziri Mkuu mpya na serikali, wakati taifa hilo la kaskazini mwa Afrika likizidi kutumbukia kwenye hali ya kisiasa isiyokua na uhakika.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Yves Le Drian, amemwambia mwenzake wa Tunisia Othman Jerandi kwamba, wananchi wa Tunisia wanasubiri hatua kama hiyo, baada ya Rais Kais Saied kufuta kazi maafisa zaidi, awali pamoja na kusitisha shughuli za Bunge  hatua ambazo wapinzani wake wamesema ni “ mapinduzi”

Akizungumza kwa njia ya simu na Jerandi, Le Drian amesisitiza umuhimu wa uteuzi wa haraka wa Waziri Mkuu na kuunda serikali ambayo itaweza kukidhi mahitaji ya wananchi wa Tunisia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa amesema.

Amesema kwamba kuna umuhimu wa kudumisha utulivu na sheria, na kuruhusu utendaji kazi wa haraka wa taasisi za kidemokrasia za Tunisia.

Mashirika muhimu ya kiraia ya Tunisia yameonya kuhusu kuongeza kinyume cha sheria muda wa siku 30 wa hatua ya rais Saied ya kusitisha shughuli za Bunge, na yameomba katika taarifa ya pamoja, ratiba ya hatua za kisiasa.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents