Michezo

Ufaransa yawa ya kwanza kutinga nusu fainali kombe la dunia

Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya kuifunga Uruguay kwa jumla ya mabao 2 – 0.

Kwa rekodi hii ya Ufaransa, Uruguay atapata tabu sana !

Kwenye dimba la Nizhny Novgorod Ufaransa imefanikiwa kuweka historia nyingine dhidi ya Uruguay baada ya mabao ya Raphael Varane dakika ya (40) na Antoine Griezmann (61) kutosha kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Dunia.

Related Articles

Back to top button