Bongo5 ExclusivesHabariMichezo

Uganda kwenye mazungumzo ya kudhamini Manchester United msimu ujao

Kupitia jarida la AFRICA FACT ZONE limeripoti kuwa Taifa la Uganda lipo kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester United ya kuitaka ilitangaze taifa hilo kimataifa.

Kupitia Wizara yao ya mambo ya Utalii taifa la Uganda limeanza mazungumzo tayari na lengo lao ni klabu ya Manchester United kulitangaza taifa hilo.

Bado haijawekwa wazi klabu hiyo italitangaza taifa la Uganda kupitia jezi au kupitia mabando ya uwanjani.

Endapo dili hilo litafanikiwa Uganda itaungana na taifa la Rwanda ambalo lipo kwenye mkataba wa muda mrefu na vilabu vya PSG na Arsenal ambapo vinavaa jezi zilizoandikwa VISIT RWANDA ambapo neno hilo limeandukwa katika jezi za timu hizo lakini pia hutolea katika mabango ya uwanjani.

Huenda jezi za Manchester za msimu ujao zikaandikwa VISIT UGANDA na pia kama iliyo kawaida baadhi ya Wachezaji wa Man United wakaenda kulitembelea taifa hilo kama ilivyo kwa Rwanda ambapo wachezaji wa PSG kama Ramos, Navas na Icardi walienda kulitembea yaifa hilo huku kwa upande wa Arsenal waliwakilishwa na David Luiz.(swippe) kuisoma taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents